Matokeo hayo yame tangazwa kutokana na orodha za Benki ya dunia kulingana na pato: 2020-2021
Tangazo lililotolewa kupitia mtandao wa Facebook kwamba Tanzania ime fikia kiwango cha nchi zenye uchumi wa kipato cha kati ni la KWELI.
Tangazo hilo linampongeza Rais John Pombe Magufuli kutokana na maendeleo ya kiuchumi nchini mwake.
Hata hivyo, mbali na kwamba orodha ya nchi zenye kipato cha kati kwenye ngazi ya chini ni moja tu miongoni mwa orodha zinazo tumiwa na Benki ya dunia, ukweli ni kwamba hakuna kabisa kiwango cha wastani katika orodha hizo.
Benki ya dunia ina kagua nchi mbali mbali kufuatana na vigezo kama vile geographia, urahisi wa kutoa mikopo, ao pia udhaifu pamoja na ukubwa wa pato la wananchi. Kutokana na msingi huo, uchumi wa nchi mbalimbali una pangwa katika makundi manne: pato la chini kabisa, pato la chini la wastani, pato la juu la wastani na pato la juu; na makundi hayo huwa haya badiliki katika kipindi cha mwaka mzima wa fedha.
Vigezo hivyo vinatangazwa kuzingatia pato la taifa na pato la kila mwananchi, katika dolla za kimarekani kulinganisha na sarafu ya Taifa katika kipimo cha Benki ya dunia kijulikanacho kwa jina la Atlas. Mambo kama vile ukuaji wa uchumi, mfumko wa sarafu,kiwango cha ubadirishaji na ukuaji wa idadi ya watu yana chukuliwa maanani ili kutangaza pato la kila mwananchi.
Kuorodheshwa Tanzania kutoka kundi la nchi zenye pato la chini sana hadi kufikia pato la kati ni tangazo lilitolewa na Benki ya dunia tarehe mosi julay, na pamoja na Tanzania, kuna nchi zingine tisa zinazo husika na tangazo hilo. Hayo yote yanatokana na kupanda kwa pato la Taifa, tokea dolla za Marekani kutoka 1.026 na kufikia hadi 3.996 kila mwananchi (hesabu za mwaka 2019).
Akizungumzia kuhusu tangazo hilo la Benki ya dunia, msemaji wa serkali ya Tanzania, Hassan Abassi, alidokeza kwamba kushuka kwa kiwango cha umaskini toka 32% hadi 28% ni moja ya sababu zilizo pelekea kufikia mageuzi hayo. Bwana Abassi aliongeza kwamba nidhamu katika matumizi ya pesa za Uma, na hali kadhalika amani inayo dumu nchini, vili changia sana kwa kufikia hatua hiyo. Kuna pia maongezeko ya uwekeshaji katika sekta za afya, elimu na pia miradi ya kujitegemea.
Tanzania ni nchi ya pili kufikia kipato cha kati miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, nchi ya kwanza iliyo tangazwa hivyo ni Kenya mwaka 2014.
PesaCheck ili chunguza uhakika wa tangazo kwamba Tanzania ime fikia kiwango cha nchi zenye kipato cha kati na kuthibitisha kwamba ni tangazo la KWELI.
TRUE: Tanzania is now a lower-middle income country

